News

KIWANGO CHA LUIS MUQUISSONE CHAWALIZA MASHABIKI AL AHLY…WADAI NI HASARA KWA TIMU…

admin December 30, 2021 3:00 pm


Licha ya Pitso Mosimane kuwapa Al Ahly taji la CAF Super Cup bado mashabiki wameendelea kumkosoa hasa baada ya Al Ahly kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Future Fc.

Mashabiki wanakosoa selection ya Kikosi kwa kuanza na Kiungo Luis Miquissone mbele ya Taher Mohamed Taher na Hussein El Shahat ambao wao wanaamini kiwango cha Luis Miquissone kinaingia zaidi ya mara milioni kwa viungo hao.

Mashabiki wanaenda mbali zaidi na kusema mpango wa kumnunua Miquissone ni uharibifu wa pesa na wana muona kama dhaifu sana.

Hata hivyo baadhi yao wamekuwa na mawazo tofauti… wengine wanamkosoa Pitso kwa kumuingiza Rami Rabia

Al Ahly wameendelea kukaa juu ya msimamo wa ligi kuu nchini Misri wakiwa na alama 19 sawa na Zamalek aliepo nafasi ya pili ila Ahly ana faida ya mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi 7 walizocheza msimu huu,Pitso amewaongoza Al Ahly kushinda michezo 6,sare 1 na hajapoteza.

BAADA YA KUTAJWATAJWA SANA KUTUA SIMBA AU YANGA …MOSES PHIRI AVUNJA UKIMYA..AFUNGUKA HAYA .. TAA YA KIJANI YAMWAKIA KIBU DENIS….KUPIGWA BEI ULAYA …MAGORI AFUNGUKA DILI LOTE A-Z…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply