Home Habari za michezo HIVI NDIVYO ‘UCHAWI’ WA CHAMA ULIVYOWARUGA WAZAMBIA WENZAKE LEO….KAZI HAIKUWA RAHISI..

HIVI NDIVYO ‘UCHAWI’ WA CHAMA ULIVYOWARUGA WAZAMBIA WENZAKE LEO….KAZI HAIKUWA RAHISI..

Habari za Simba

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Clatous Chama ameisaidia timu yake kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akifunga yote mawili.

Simba imeanzia hatua ya pili ya mashindano hayo na hivyo inasubiri mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba Mosi, ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi.

Viwango vya timu hizo havikutofautiana sana katika mchezo huo uliopigwa mjini Ndola, Zambia licha ya Dynamos kuanza kucheka na nyavu, na Simba kusawazisha timu hizo zilishambuliana kwa zamu huku zikijilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

Dynamos ndio ilianza kupata bao katika dakika ya 28 lililofungwa na Joshua Mutale aliyepiga krosi na beki wa Simba, Henock Inonga ni kama alipoteza mwelekeo, ambapo kipa Ayoub Lakred ameugusa mpira kwa kisigino kabla ya kuingia nyavuni.

Simba ilisawazisha bao hilo dakika ya 59 baada ya Beleke kupiga mpira kutokea pembeni pasi iliyomkuta Yassin Mzamiru aliyepiga shuti kali ambalo kipa Mulenga Lawrence ametema na Chama kuuwahi kisha kufunga.

Dakika ya 74 Dynamos ilipata bao la pili kupitia kwa Aaron Katebe aliyepiga shuti kali, ambapo kipa wa Simba, Ayoub alidaka na mpira kumponyoka kisha kujaa kwenye nyavu zake.

Simba ilibadili matokeo katika dakika za jioni, Chama akifunga bao la pili dakika 90+3 na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya mabao 2-2.

SIMBA DAY

Kwenye tamasha la Simba Day ilialikwa Dynamos, ikachapwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo mchezo wa leo timu hizo hazikuwa na ugeni kwani zinajuana.

Kikosi cha Simba kilichoanza leo kilikuwa na Ayoub Lakred, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Che Malone, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Kibu Denis, Mzamiru Yassin, Moses Phiri, Clatous Chama na Willy Onana.

Benchi kuliwakuwa na Ally Salim, Hussein Abel, Israel Mwenda, Kennedy Juma, Fabrice Ngoma, Said Ntibanzokiza ‘Saido’, Luis Miquissone, Jean Baleke na John Bocco.

SOMA NA HII  RASMI...SIMBA SC KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI NA MABINGWA WA UEFA...RATIBA NZIMA HII HAPA...