Home Ligi Kuu 10 BORA NDANI YA LIGI KUU BARA HIZI HAPA

10 BORA NDANI YA LIGI KUU BARA HIZI HAPA


LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 27 ambapo ile burudani ambayo ilikuwa kimya kwa muda mrefu inarejea kwa kasi na kila timu ikiwa inahitaji kufikia malengo yake.

Hapa leo tunajikumbusha timu 10 bora ambazo ziliweza kufanya vizuri na kwa zile ambazo zilipanda ligi ni Dodoma Jiji iliweza kufanya vizuri na kuwa ndani ya 10 bora kwa mara ya kwanza na inanolewa na Kocha Mkuu Mbwana Makata.

Ukianza kwenye namba moja ipo mkononi mwa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wananolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes  huyu mwamba ni raia wa Ufaransa alifanya kazi na mzawa Seleman Matola.

Ilikuwa hapo baada ya kukusanya jumla ya pointi 83 kibindoni na ilicheza jumla ya mechi 34, ilishinda mechi 26, sare 5 na ilipoteza mechi tatu ndani ya ligi.

Namba mbili ipo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi huyu ni raia wa Tunisia ni pointi 74 ilikusanya katika mechi 34 ilishinda mechi 21, sare 11 na ilipoteza mechi mbili msimu uliopita.

Matajiri wa Dar hawa ni Azam FC ilijichimbia nafasi ya tatu baada ya kusepa na pointi 68 ilishinda mechi 19, sare 11 na ilinyooshwa katika mechi nne.

Wanajeshi wa Mpakani ni Biashara United nafasi ya nne , ilikusanya pointi 50, ushindi mechi 13,sare 11 ilionja joto ya jiwe katika mechi 10.


Tano wanajiita Wanakino Boys, KMC pointi zao ni 48, ilipoteza mechi 12,sare 9 ushindi ilikuwa mechi 13 kwa msimu wa 2020/21 ndani ya ligi.

Waite Polisi Tanzania hawa walikuwa nafasi ya sita baada ya kukusanya pointi zao 45 ilipoteza mechi 9,sare 15 na ushindi ni katika mechi 10.

Saba kama saba imekaa kwa Tanzania Prisons wazee wa pira gwaride, walikusanya pointi 44, ushindi ilikuwa mechi 10,sare 14 na kupoteza mechi 10.

Wakali Dodoma Jiji wazee wa pira Zabibu walikusanya pointi 44,ushindi mechi 11 sare 11 na kupoteza mechi 12.Hawa ikumbukwe kwamba ilikuwa ni msimu wake wa kwanza na ikafanya vizuri pia.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE - SIMBA WAACHANE NA RALLY BWALYA..ANACHEZA SOKA LAINI, HANA MAAMUZI YA HARAKA...

Tisa ni Namungo pointi 43,ushindi mechi 10,sare 13 kichapo mechi 11 na namba 10 ipo mikononi mwa Mbeya City, pointi zao ni 42, ushindi mechi 10, sare 12 kichapo 12.