Home Azam FC NDEGE MPYA YA AZAM FC INAYOTEMBEA ARDHINI KUPITA KWA MWENDO WA TARATIBU

NDEGE MPYA YA AZAM FC INAYOTEMBEA ARDHINI KUPITA KWA MWENDO WA TARATIBU


MENEJA Masoko na Mauzo wa Azam FC, Tunga Ally, leo Alhamisi Oktoba 7 ameongoza zoezi la makabidhiano ya basi jipya la Azam FC ambalo wao wanaita ndege ya ardhini.

Gari hilo matata na bora ni Mercedes Benz Irizar i6S Plus ambapo makabidhiano yamefanyika kwa dereva mpya atakayeendesha basi hilo (mwenye bluu) mpaka Dar es Salaam. 

Dereva aliyelitoa basi hilo nchini Afrika Kusini, alimkabidhi funguo dereva mpya, kwa ajili ya kuanza safari ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ndiga hiyo itakuwa katika mwendo wa kawaida ili kuwaruhusu mashabiki wa Azam FC kuweza kuliona basi hilo.

Dereva ambaye amekabidhiwa basi hilo ataendelea na safari ya kuibuka Dar  kupitia miji ya Mbeya, Iringa na Morogoro.

Tunga pia aliwakabidhi madereva wote jezi mpya za Azam FC zenye ubora mkubwa wa kimataifa.

SOMA NA HII  KISA CHAMA NA BWALYA...PABLO ATIKISA KICHWA KISHA ANENA HAYA...ATANGAZA HATARI...