Home Habari za michezo KUISHUHUDIA SIMBA VS ASEC NI BUKU 5 TU

KUISHUHUDIA SIMBA VS ASEC NI BUKU 5 TU

Klabu ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa siku ya Novemba 25, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klanbu ya Simba, Ahmed Ally, amebainisha kuwa viingilio kwa mzunguko ni Tsh 5000, VIP C Tsh 10,000, VIP B Tsh 20,000, VIP A Tsh 30,000 huku viingilio kwa Platinum vikiwa Tsh 150,000.

Miamba hiyo ya Ivory Coast inatarajiwa kutua Nchini Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni watatoka Nchini Misri.

SOMA NA HII  HUYU HAPA KAPOMBE....YANGA MJIANDAE KUITA MAJI 'MMA' HIYO JUMAPILI...