Home Uncategorized AZAM FC YAFUNGA DIRISHA DOGO NA MAJEMBE HAYA YA KAZI

AZAM FC YAFUNGA DIRISHA DOGO NA MAJEMBE HAYA YA KAZI


 KIKOSI cha Azam FC kimefunga usajili wa dirisha dogo kwa kuinyaka saini ya kiungo mshambuliaji, Yahya Zayd, kwa mkopo wa miezi sita akitokea Pharco ya Misri.

Zayd ni mmoja wa wachezaji waliokulia kwenye kituo cha Azam Academy kabla ya kumpandisha timu kubwa ya Azam FC na aliuzwa katika Klabu ya Ismaily ya Misri 2018.

Kiungo huyo mshambuliaji anfunga usajili wa dirisha dogo akiungana na mshambuliaji Mpiana Monzinzi (Congo DR) na kipa Mathias Kigonya (Uganda).

Azam imeachana na kiungo mshambuliaji Richard Djod mzee wa udambwiudambwi ambaye ameachwa ili kupisha nafasi ya kipa Kigonya.


Awali ilikuwa inaelezwa kuwa kipa namba moja David Kissu angetolewa kwa mkopo ila mambo yamekuwa tofauti baada ya Kocha Mkuu, George Lwandamina kuamua abaki ndani ya timu hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa malengo ya Azam FC ni kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.
SOMA NA HII  ISHU YA DUKA LA JEZI SIMBA WAIJIBU YANGA, WATAJA WASHINDANI WAO NI WAARABU