Home Habari za michezo BAADA YA KUKOSA UBINGWA…SIMBA WATAKA KIATU CHA MFUNGAJI BORA KUJIFARIJI…

BAADA YA KUKOSA UBINGWA…SIMBA WATAKA KIATU CHA MFUNGAJI BORA KUJIFARIJI…

Habari za Michezo Leo

Baada ya kiungo wa Simba, Saido Ntibazonkiza kumsogelea kwa ufungaji mshambuliaji Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 na yeye 15, uongozi wa Simba umetoa neno.

Simba jana Juni 6 ilishinda mabao 6-1 huku Saido akiweka wavuni mabao 5 akipaa kutoka 10 hadi 15.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakitaka kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2022/23 na mechi ya mwisho ya msimu watamsaidia Saido ili akibebe.

Ligi Kuu Bara imebaki mechi moja kutamatakika ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union Dar na Yanga itacheza dhidi ya Tanzania Prisons Sumbawanga.

“Tunahitaji mfungaji bora, zimesalia bao 2 na hakuna mashaka kwenye mechi ya mwisho ya Coastal tutamsaidia timu nzima awe mfungaji bora,” amesema Ahmed na kuongeza;

“Uliona kuna nafasi John Bocco alikuwa nafasi ya kufunga akasema hii ya Saido akamwekea akafunga, bao la tano alikuwa na uwezo wa kufunga Kibu lakini akamtengea Saido,”

SOMA NA HII  HIZI HAPA BILIONI 80 ZA MERIDIANBET ZINAKUNGOJA....KUSHINDA NI RAHISI MNOOOO....