Home Habari za michezo NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA…HAKUWA BORA KWANGU …

NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA…HAKUWA BORA KWANGU …

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga Nasreddine Mohammed Nabi, ametetea maamuzi yake ya kumtoa Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephen Aziz Ki, wakati wa mchezo wa mzunguuko wanne wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya AS Real Bamako ya Mali.

Katika mchezo huo Yanga ilicheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kuchomoza na ushindi wa 2-0, ambao unaiweka katika nafasi nzuri ya kutinga Hatua ya Robo Fainali.

Nabi amesema maamuzi ya kumtoa Aziz Ki baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo, yalitokana na mfumo ambao alilazimika kuutumia wakati wa kipindi cha pili.

Amesema hakuna asiyefahamu uwezo wa mchezjai huyo, lakini linapokuja suala la mfumo, hana budi kumtumia mchezaji mwingine kwa maslahi ya Yanga.

β€œWote tunakubaliana na ubora wa Aziz, ni mchezaji mzuri, lakini unaweza kuwa mchezaji mzuri ila usipofuata mfumo timu inavyocheza unakuwa unaonekana sio bora” amesema Nabi

Ushindi wa 2-0 dhidi ya AS Real Bamako unaendelea kuiweka Yanga katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, ikifikisha alama 07 nyuma ya US Monastir iliyofikisha alama 10 baada ya kuifunga TP Mazembe ya DR Congo 1-0 jana Jumatano (Machi 08).

TP Mazembe ipo nafasi ya tatu ikiendelea kuwa na alama zake 03, huku AS Real Bamako ikiwa na alama 02.

SOMA NA HII  HUKO YANGA UNAAMBIWA UBABE UBABE TU