Home Azam FC AZAM FC KAZINI LEO HATUA YA 16 BORA MBELE YA POLISI TANZANIA

AZAM FC KAZINI LEO HATUA YA 16 BORA MBELE YA POLISI TANZANIA


 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Aprili 28 kina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ni wa hatua ya 16 bora na yule atakayepoteza safari yake ya kulisaka taji hilo itakuwa imefika kikomo.

Kwa sasa mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni Simba ambao walitwaa taji hilo zama za Sven Vandenbreocek kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Songea na safari hii fainali itapigwa Kigoma.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo yao ni kuona kwamba wanapata ushindi kwenye mchezo huo ili kuweza kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa.

“Tupo imara na tunahitaji kurejea katika mashindano ya kimataifa, ili uweze kurudi huko ni lazima upate ushindi na kutwaa taji tunaamini tutafanya vizuri, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  AZAM FC WAFUNGUKIA ISHU YA KUMVUTA KWENYE BENCHI LA UFUNDI KOCHA MRUNDI