Home Habari za michezo ISHU YA MKATABA WA CHAMA NA SIMBA….. UKWELI WOTE HUU HAPA…

ISHU YA MKATABA WA CHAMA NA SIMBA….. UKWELI WOTE HUU HAPA…

Habari za Simba leo

Maswali yaliyopo vichwani kwa mashabiki na wadau wa soka nchini ni kuhusu hatima ya kiungo fundi wa Simba, Mzambia, Clatous Chama. Je ataachwa? Atabaki? Wengi wanajiuliza hivyo, lakini majibu ya  ishu nzima iko hivi.

Ni kweli mkataba wa Chama na Simba unafika kikomo mwisho wa msimu huu na awali viongozi wa timu hiyo walikubaliana kuachana na kiungo huyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mambo ya kinidhamu.

Hata hivyo, vigogo hao wameingia ubaridi katika maamuzi hayo baada ya kiwango bora anachokionyesha Chama tangu alivyorejea kutoka kutumikia kifungo cha utovu wa nidhamu.

Ikumbukwe, Desemba 21, mwaka jana Chama na mwenzake Nassoro Kapama walisimamishwa na uongozi wa Simba kwa makosa ya kinidham

Inafahamika Chama alipishana kauli na kocha wa viungo wa timu hiyo Kamal Boudjenane jambo ambalo lilimboa Kocha mkuu Abdelhak Benchikha na Kuumbia uongozi umchukulie hatua na kweli ukamsimamisha.

Januari 29, mwaka huu Simba ilimsamehe Chama na hiyo ni baada ya staa huyo kuomba radhi kwa uongozi na benchi la ufundi na wote kumaliza tofauti kisha akarejea kikosini na kuanza kucheza bila bifu na mtu yeyote.

Tangu alivyorejea kikosini hapo Chama amekuwa na kiwango bora na kuhusika kwenye mabao sita kati ya 14 iliyofunga Simba kwenye mechi tano za ligi na mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga mabao matatu na kutoa asisti tatu.

Kiufupi karibu nusu ya mabao yote iliyoyafunga Simba kwenye mechi hizo saba yalitokea kwa Chama. Hapo mechi ya jana haipo.

Hivyo hilo limeushitua uongozi na ghafra kuanza kuwaza kuandaa mkataba mpya wa kiungo huyo ambaye kwa mara ya kwanza alisajiliwa na Simba mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya kwao Zambia na kudumu hadi 2021 alipouzwa kwenda RS Berkane ya Morocco lakini akarejea tena Simba mwaka 2022.

Moja ya viongozi wa ngazi za juu Simba (jina tunalo), amesema kuwepo na presha kuhusu kumuongezea mkataba mpya Chama lakini uongozi umemwachia jukumu hilo, kocha Benchikha.

“Ungekuwa wewe ungemuacha aondoke?” Aliuliza kiongozi huyo na kuongeza; “Ni kweli kuna presha juu ya jambo hilo lakini sisi tunaamini hatutashindwa kitu.

Kwa sasa jambo la kumuongezea mkataba mpya Chama tumemuachia kocha mkuu (Benchikha), yeye ndio ataamua kutokana na mahitaji yake ya kikosi kwa msimu ujao. Kwa sasa mashindano mengi yanaendelea, suala la usajili hatuliwazi sana kwani nguvu nyingi ipo kwenye mashindano lakini wakati ukifika kila jambo litakaa sawa na tutazingatia zaidi ripoti ya benchi la ufundi kwani wachezaji wengi mikataba yao inatamatika msimu huu,” alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo Chama hadi kufika jana alikuwa hajazungumza na uongozi kuhusu kuongeza mkataba mpya na za chini chini kutoka kwa watu wa karibu na staa huyo, anasubiri akiwashe zaidi katika mechi zilizobaki kwa msimu huu ili akikaa mezani na Simba basi thamani yake iwe juu.

Aidha vyanzo hivyo vinaeleza, Chama ana ofa mbili nje ya Tanzania, lakini bado anapendelea kuendelea kucheza soka Tanzania kutokana na upendo wake kwa nchi hii, pia mazingira mazuri kwa familia yake kwani watoto wake wanasoma Dar es Salaam lakini pia anaishi na mpenzi wake hapa.

Kabla ya mechi ya juzi, Chama alikuwa amefunga mabao manne kwenye ligi na kutoa pasi za mwisho ‘asisti’ tatu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUICHARANGA KMC KWA HASIRA JUZI...MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ALICHOKIONA...ADAI WALISUMBUA...