Home Habari za michezo MWASITI AKIRI WAZI WAZI MOYONI KWAKE…ANA HIP-HOP NA SIMBA SC TU

MWASITI AKIRI WAZI WAZI MOYONI KWAKE…ANA HIP-HOP NA SIMBA SC TU

MWASITI AKIRI WAZI WAZI MOYONI KWAKE...ANA HIP-HOP NA SIMBA SC TU

NI zaidi ya miaka 15 sasa anaitumikia Bongofleva kwa maslahi mapana ya mashabiki wake, ana sauti ya kuvutia, anajua kucheza na jukwaa na anapendwa na wengi kutokana na muziki na mtindo wake wa maisha.

Mwasiti ameshinda tuzo, amefanya shoo kubwa za ndani na nje kama Malaria No More Benefit Concert (New York) na ametoa EP, The Black Butterfly (2021), huyu ndiye Mwasiti Almas;

1. Mwasiti alianza kujihusisha na muziki akiwa na miaka tisa tu, hiyo ilikuwa mwaka 1995 ila wimbo wake wa kwanza uliokuja kumtoa kimuziki ‘Niambie’ ulitoka mwaka 2006 ikiwa ni miaka 11 tangu kuanza kuimba.

2. Huyu ndiye msaniii wa kwanza wa kike Bongo kutajwa kuwania vipengele vitano katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2013, utakumbuka tuzo za KTMA ndio hizo sasa zilizolirudia jina lake la awali zikijulikana kama TMA (Tanzania Music Awards).

Aliwani kama Msanii Bora wa Kike, Msanii Bora wa Kike Bongofleva, Wimbo Bora wa Kushirikiana (Mapito ft. Ally Nipishe), Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba (Mapito) na Wimbo Bora wa Mwaka (Mapito), lakini hakushinda hata moja!.

3. Barnaba alikuwa akienda Tanzania House of Talent (THT) na nguo za shule ili kutafuta njia ya kuonyesha uwezo wake na kutoka kimuziki, wakati huo Mwasiti ndiye aliyekuwa Jaji wa THT na alimpa nafasi na mengine sasa ni historia tu.

4. Mwaka 2007 ndipo Mwasiti alishinda tuzo yake ya kwanza katika muziki, ni kutoka KTMA kama Msanii Bora Chipukizi akiwa ndiye msanii wa kwanza wa THT kubeba tuzo hiyo.

Wasanii wengine ambao wamewahi kushinda tuzo ya msanii chipukizi ni Diamond Platnumz (2010), Linah (2011), Ommy Dimpoz (2012), Ally Nipishe (2013), Young Killer (2014), Barakah The Prince (2015), pia kuna Rapcha na Phina (2022).

5. Wimbo wa Mwasiti ‘Sio Kisa Pombe’ akimshirikisha Quick Rocka uliandikwa na Barnaba, huku wimbo wake ‘Bado’ akimshirikisha Billnass ukiandikwa na Marioo, ila Quick Rocka na Billnass waliandika verse zao wenyewe.

6. Godzilla ndiye rapa pekee Bongo ambaye Mwasiti amefanya naye ngoma nyingi, nne ikiwa ni sawa na Mwana FA na Lady Jaydee, Stamina na Maua Sama ambao wote pia wamefanya kolabo zaidi ya nne.

7. Mwaka 1995 ndipo mama yake alibaini kuwa Mwasiti ana kipaji cha kuimba, hata alipotoka na kuwa msanii mkubwa bado mama yake alikuwa ndiye anamshauri katika uandishi wa nyimbo zake na kupendekeza wimbo upi unaweza kutoka kwa wakati husika.

8. Kolabo bora ya Chid Benzi kwa muda wote ni yake na Mwasiti ‘Hao’ iliyotoka mwaka 2007 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza kutoka KTMA 2006 kama Msanii Bora wa Hip Hip kufuatia kufanya vizuri kwa ngoma yake, Naitwa Nani akimshirikisha K-Lyyn.

9. Mwasiti amekuwa kipenzi cha muziki wa Hip Hop, miongoni mwa wasanii wa Rap aliowahi kuwashirikisha kwenye nyimbo zake ni Chid Benzi (Hao), Quick Rocka (Sio Kisa Pombe), Godzilla (Soldier & Leo), Billnass (Bado) na Roma (Fall in Love).

Wasanii wa Hip Hop waliowahi wakumpa shavu Mwasiti katika ngoma zao ni D Knob (Nishike Mkono), Lord Eyes (Kwanini), Izzo Bizness (Walala Hoi) na Godzilla (First Class & Genius).

10. Mwasiti ambaye ni shabiki wa Simba SC, wimbo wake ‘Nalivua Pendo’ ndio wenye mafanikio zaidi kwake kwani ulikaa kwenye chati za Radio kwa zaidi ya wiki nane, huku ukishinda tuzo ya KTMA 2009 kama Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba. Na wimbo huo Mwasiti aliandikiwa na Mzee Abuu wa Kariakoo.

SOMA NA HII  CHAMA AFUNGUKA KUHUSU HESHIMA YA SIMBA, ATAKA JAMBO HILI MSIMU HUU KWA SIMBA