Home Habari za Simba Leo PRINCE DUBE AMTAJA CHAMA NA AZIZ KI

PRINCE DUBE AMTAJA CHAMA NA AZIZ KI

habari za yanga leo-AZIZ KI

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube ameweka wazi kuwa kucheza timu moja na wachezaji wenye uwezo ikiwa ni Clatous Chama, Aziz Ki kunamuongezea hali ya kujiamini na kupambana zaidi.

Dube ingizo jipya ndani ya Yanga kwenye eneo la ushambuliaji utambulisho wake ulifanyika usiku wa Julai 7 ikiwa ni zawadi ya 7/7 kwa Wananchi.

Katika mchezo wa Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini ikiwa ni maandalizi ya msmu wa 2024/25 Dube alifunga bao moja la ufunguzi kwenye mchezo huo.

Baada ya dakika 90 ilikuwa Kaizer Chiefs 0-4 Yanga wakitwaa taji hilo na tayari wamesharejea Dar kwa maandalizi ya Wiki ya Mwananchi ambapo kilele chake inatarajiwa kuwa Agosti 4 na Yanga itacheza dhidi ya Red Arrows.

Dube amesema: β€œKucheza timu moja na Chama, Aziz na wachezaji wengine hii kwangu ni furaha kwani hawa ni wachezaji wenye uwezo na wanaongeza nguvu ya kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri.”

SOMA NA HII  KIUNGO SIMBA ATAMBULISHWA BURUNDI