Home Habari za Simba Leo SALEH JEMBE ATAJA SIFA ZA JOSHUA MUTALE…USAJILI MZURI KWA SIMBA

SALEH JEMBE ATAJA SIFA ZA JOSHUA MUTALE…USAJILI MZURI KWA SIMBA

Habari za Simba- Mutale

MCHAMBUZI NGULI wa Michezo Saleh Ally Jembe ni miongoni mwa wale waliokuwa Misri kushuhudia maandalizi ya Simba kuelekea kwenye Ligi Kuu Bara 2024/25 Jembe amezungumzia mchezo mzima kwa kuandika namna hii kuhusu Winga wa Simba Joshua Mutale.

Kisukuma Mutale, maana yake ni mkubwa, ila unatakiwa kuivuta kidogo Mutaale…
Huyu Mutale wa Simba kiumbo si mkubwa lakini mambo yake ni makubwa na atakuwa gumzo ninaamini.

Kasi…nguvu…si mwoga na ana uwezo wa kuwatambuka hata walinzi watatu… Lakini hatari zaidi anapiga mashuti…

Mfano bao la pili la Simba dhidi ya Wasaudi, alipokea mpira pembeni, akatembea kwa kasi na kupiga shuti kali sana…Likagonga mwamba na kurudi ndani.

Wakati walinzi wanajishauri kwa kasi yake alishafika na kupiga shuti tena…BAOO.

Anyway ni mchezaji ambaye inaweza kuwa moja ya KARATA BORA WALIZOPATA SIMBA na ITACHANGIA WAREJEE…

SOMA NA HII  KUELEKEA 'KARIKAOO DERBY'...BENCHIKHA AWAPA KISOMO MASTAA WOTE SIMBA...