Home Habari za Simba Leo MUKWALA NA MUTALE WAFUNGUKA A-Z KAMBI YA SIMBA

MUKWALA NA MUTALE WAFUNGUKA A-Z KAMBI YA SIMBA

Habari za Simba- Joshua Mutale

WACHEZAJI Wapya wa Simba Joshua Mutale winga na Steve Mukwala Mshambuliaji wamefunguka kuelezea namna ambavyo kambi ya timu hiyo ilivyokuwa huko Ismailia Misri.

Akizungumzia kikosi chao, Joshua Mutale alisema walikuwa na muda mzuri Misri kujiweka sawa tayari kwa msimu mpya huku akidai kuwa wamejengeka kimwili na kiushindani.

Alisema wamepata utimamu wa mwili vizuri na wapo tayari kwa kushindana huku akifurahia namna wachezaji wenzake walivyo na muunganiko mzuri.

Kwa upande wa Steve Mukwala ambaye alifunga goli moja kwenye mchezo wa mwisho wa kirafiki alisema, walikuwa na maandalizi mazuri na ameona namna wachezaji wenzake walivyokuwa wanapambana kusaka nafasi kikosi cha kwanza.

“Kwa upande wetu kama wachezaji tunafikiri kuna kitu tumeongeza hasa kwenye mechi tatu tulizocheza, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona timu yao Jumamosi katika Simba Day, nawaahidi kuwa watafurahi,” alisema.

Katika mechi tatu walizocheza Simba wakiwa Misri, wamefunga mabao saba na kuruhusu mawili. Wafungaji wao ni Mutale, Mukwala, Mashaka, Ladack Chasambi, Augustine Okejepha na Charles Ahoua aliyepiga mbili

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA...HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUENDELEA NA MGUNDA...