Home Habari za michezo RASMI….IBENGE AFUNGUKA A-Z CHANZO CHAMA NA KISINDA KUSHINDWANA NA WAMOROCCO…

RASMI….IBENGE AFUNGUKA A-Z CHANZO CHAMA NA KISINDA KUSHINDWANA NA WAMOROCCO…

Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Hilal ambaye amewahi kuifundisha RS Berkane ya Morocco Florent Ibenge, amefunguka sakata la kiungo mshambuliaji, Tuisila Kisinda alivyoondoka klabuni hapo.

“Clatous Chama aliondoka RS Berkane mapema kabla mimi sijaondoka lakini mimi niliondoka nikamwacha Tuisila Kisinda.

“RS Berkane walitaka kumtoa Kisinda kwa mkopo (palepale Morocco) kwa sababu walikuwa wamesajili washambuliaji wengi lakini sio kwa sababu mimi nilikuwa nimeondoka.

“Kitu kingine ni kwamba, Kisinda hakuwa sehemu ya kikosi cha Berkane wakati wa Pre-season kwa sababu alikuwa Kinshasa anashughulikia masuala ya hati yake ya kusafiria ilikuwa na changamoto kidogo.

“Kocha mpya hakupendezwa na kitendo cha Kisinda kuchelewa kujiunga na timu… kwenye Pre-season akashauri atolewe kwa mkopo, Kisinda akaamua kuomba kuondoka,” amesema Florent Ibenge.

Kisinda kwa sasa amerejea Yanga aliyoitumikia kwa msimu mmoja wa mwaka 2020/2021 wakati huo Ibenge akiwa na kibarua cha kuizuia Yanga kupasua ngome yake Jumapili ijayo katika mechi ya marudiano ya kuwania kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  KUHUSU MABADILIKO YA SHERIA KWA WACHEZAJI WOTE WA KIGENI KUTUMIKA MSIMU HUU WA LIGI KUU...UKWELI HUU HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here