Home Habari za michezo YANGA YAMFUNGA MABOMU MORISSON….APIGISHWA TIZI LA HATARI KUWAUA SIMBA

YANGA YAMFUNGA MABOMU MORISSON….APIGISHWA TIZI LA HATARI KUWAUA SIMBA

NABI AKABIDHIWA BERNARD MORISSON...YANGA YA MOTO AKOSA NAMBA

YANGA ina akili sana. Wakati juzi ikikamilisha ratiba ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kucheza na TP Mazembe, jijini Lubumbashi DR Congo, benchi lake la ufundi limeanza mapema kusuka mipango ya kuicheza Kariakoo Derby itakayopigwa Aprili 16 kuanzia saa 11:00 Kwa Mkapa.

Moja na mikakati hiyo ni kumuandalia programu maalumu kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Bernard Morrison ‘BM33’, ili awe fiti ili kuimaliza Simba kwenye pambano hilo litakalokuwa la 110 tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.

Yanga ilimwacha Morrison, jijini Dar es Salaam makusudi ili aendelee na programu maalumu ya kumfanya awe fiti zaidi baada ya kupona jeraha lake la nyonga lililomweka nje kwa zaidi ya mwezi, lakini SOKA LA BONGO limepenyezewa, mpango huo ni mkakati wa benchi la ufundi ili kumtumia kwenye mechi mbili zijazo za Yanga pamoja na ile na Kariakoo Derby.

Chanzo chetu kilisema benchi la ufundi la Yanga chini ya Kocha Nasreddine Nabi aliyeko Ubelgiji akifuatilia hati ya kusafiria, limemwandaa kiaina Morrison kuivaa Simba kutoka na uzoefu na Derby huku akipewa mechi ya Kombe la ASFC dhidi ya Geita Gold itakayopigwa Jumamosi kisha ya ligi dhidi ya Kagera ni April 11, mwaka huu.

“Kocha mkuu ndiye alipendekeza tusisafiri naye kuja DRC kwa sababu ana mpango naye.

Anataka amtumie katika mechi mbili zijazo, ile apate utimamu wa mchezo ‘Game Fitness’ na kama ataonekana kuwa tayari basi huenda akaanza naye rasmi dhidi ya Simba kwani anaamini ni aina ya wachezaji wanaoziwezea mechi za Dabi,” kilieleza chanzo chetu.

Hata hivyo, katika moja ya mahojiano ya Nabi na gazeti hili alisema anamsikilizia Morrison awe fiti kwa kiwango atakachoridhika na baada ya hapo ataanza kumtumia.

“Morrison aliumia na alipopona akatukuta tupo kwenye mechi za CAF zilizohitaji wachezaji waliofiti kwa asilimia zote, hiyo ndio sababu kuu hatujamtumia ila siku si nyingi mtamwona,” alisema Nabi.

Morrison kwa msimu huu hadi sasa ameichezea Yanga mechi 10 tu za ligi na kufunga mabao mawili na asisti tatu, huku zile za kimataifa akicheza mbili tu.

SOMA NA HII  INONGA ALISTAHILI JAMBO HILI