Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI…HAYA HAPA MANUFAA YA YANGA KUONGOZA KUNDI LAO….CAF WAANZA KUITOLEA...

KAMA ULIKUWA HUJUI…HAYA HAPA MANUFAA YA YANGA KUONGOZA KUNDI LAO….CAF WAANZA KUITOLEA MACHO…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga wametengeneza mahesabu makubwa sana kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Afrika kwa kumaliza kinara wa kundi lake akiwa na alama 13.

Jambo hilo ni historia kwao na kwa Taifa kwa ujumla licha ya kwamba Simba aliwahi kuongoza Kundi Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Al Ahly.

Kwenye mahesabu wamepata faida mbili kubwa, Yanga wamepata faida ya kwanza ni kutokutana na waliomaliza nafasi ya kwanza katika makundi ikiwa watamaliza hivyo.

Fadida ya pili ni kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani mchezo wa robo fainali. Sio kila klabu imeweza msimu huu.

Yanga imechukua alama 6 muhimu kwa TP Mazembe na kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kupata ushindi kwenye dimba la TP Mazembe. Yanga wameonesha kuwa wao ni bora sana popote wana shinda.

Yanga inatengeneza bond kubwa na CAF kwa kasi mno. Jitihada za GSM, wanachama mpaka mashabiki wameamua kuwa pamoja kutafuta mafanikio zaidi kimataifa, wachezaji wanajituma sana dimbani.

TP Mazembe walifanya kila kitu lakini Young Africans walifanya kila kitu kwa usahihi! approach nzuri imewapa matokeo. Yanga wamefanya vizuri sana kwenye hatua ya Makundi, hii ni kutokana na ubora wa kikosi chao.

SOMA NA HII  MAPINDUZI BALAMA, DICKSON JOB KAMILI GADO KWA KAZI YANGA