Home Uncategorized MWAMNYETO, NYOTA ANAYEWINDWA NA SIMBA NA YANGA ATOA YA MOYONI

MWAMNYETO, NYOTA ANAYEWINDWA NA SIMBA NA YANGA ATOA YA MOYONI

BEKI Chipukizi anaye

kipiga ndani ya Coastal Union, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa ikitokea amepata dili la kujiunga ndani ya Simba ama Yanga atacheki maslahi ili akapige kazi kwenye timu hizo.


Sarakasi za kuipata saini ya Mwamnyeto imekuwa ikiripotiwa mara nyingi ambapo Simba inaelezwa kuwa wapo mstari wa mbele kuipata saini yake na Yanga pia wakiwa karibu na nyota huyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwamnyeto amesema kuwa amekuwa akiskia juu ya yeye kuhusishwa kutua ndani ya klabu za Kariakoo jambo ambalo linamfanya asubiri mambo yatakuaje.

“Kwa sasa nimekuwa nikiskia juu ya mimi kuhitajika kutua kwenye klabu hizo ila sina mashaka na uwezo wangu ninajiamini, kikubwa ni utaratibu ufuatwe ili nitue ndani ya klabu yoyote ambayo inanihitaji,” amesema.

Safu ya ulinzi ya Coastal Union ipo nafasi ya pili kwa kuruhusu mabao machache ikiwa inaongozwa na Mwamnyeto ikiwa imefungwa mabao 19 kati ya mechi 28 ikwa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo.
SOMA NA HII  MCHEZO MZIMA WA YANGA KUICHAPA BAO 1-0 MTIBWA SUGAR ULICHEZWA HIVI