Home Uncategorized MCHEZO MZIMA WA YANGA KUICHAPA BAO 1-0 MTIBWA SUGAR ULICHEZWA HIVI

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUICHAPA BAO 1-0 MTIBWA SUGAR ULICHEZWA HIVI

 


MABINGWA wa kihistoria ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga jana wameibuka wababe mbele ya Mtibwa Sugar ambao waliikazia Simba walipokutana kwa ambapo walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1

Jana Yanga ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu mazima Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilipachikwa kimiani na Lamine Moro beki kisiki wa Yanga kwa kona iliyopigwa na Muangola, Carlos Carinhos ambaye jana alianza kikosi cha kwanza mara ya kwanza akitumia dakika 72.


Ushindi huo unakuwa ni wa tatu kwa Yanga kushinda ambapo, wapinzani wao Simba wanaokutana nao Oktoba 18 walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar hivyo jana Yanga waliwajibu kibabe.

Moro amekuwa na maelewano mazuri na Carlos ambapo amefunga mabao mawili ndani ya ligi akimalizia kona inayopigwa na nyota huyo lile la kwanza aliwafunga Mbeya City Uwanja wa Mkapa na kumfanya awe kinara wa utupiaji ndani Yanga akiwa ametupia mabao mawili.

Mfungaji wao wa kwanza kwenye ligi akiwa na bao moja alilowatungua Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa msimu wa 2020/21 Michael Sarpong alibanwa mbavu na beki chipukizi wa Mtibwa Sugar, Dickson Job ambaye alipewa kazi maalumu ya kwenda naye sambamba mwanzo mwisho.

Beki wa zamani wa Yanga, Hassan Kessy jukumu lake lilikuwa kupambana na Carlos ambaye alionekana kupambana ndani ya dakika 72 alizotumia na dakika ya 41 alimchezea rafu Kessy katika harakati za kuokoa mpira.

Yanga inafikisha jumla ya pointi 10 sawa na Simba inakuwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, Yanga imefunga mabao manne na Simba imefunga mabao 10.

Yanga imeshinda mechi tatu mfululizo za ligi ilikuwa mbele ya Mbeya City kisha ikaibukia Kagera Sugar na jana imeshinda mbele ya Mtibwa Sugar na kote ikiwa ni mwendo wa mojamoja.Mtibwa Sugar inapoteza mchezo wa kwanza ikiwa nyumbani kwa msimu wa 2020/21 baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting pamoja na sare mbele ya Simba.

SOMA NA HII  WACHEKA NA NYAVU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND HAWA HAPA