Home Uncategorized KOCHA SIMBA APATA DILI LA MIAKA MITATU AFRIKA KUSINI

KOCHA SIMBA APATA DILI LA MIAKA MITATU AFRIKA KUSINI

 


BLACK Leopard ya Afrika Kusini imempa dili la miaka mitatu, Patrick Aussems kukinoa kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Aussems raia wa Ubelgiji alikuwa Kocha Mkuu wa Simba alipigwa chini mazima msimu wa 2019/20 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Akiwa Simba aliweza kutwaa taji ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 na alifanikiwa kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Anatarajiwa kuwasili nchini Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kipya.
 
Aussems ameiambia City Press kuwa :”Muda mrefu nilikuwa nahitaji kufanya kazi Afrika Kusini, ninafuraha ya kupata kazi huko ninaamini nitafanya vizuri.

“Ligi ya Afrika Kusini imekuwa kubwa na ni maarufu ukianzia kwenye miundombinu mpaka ukusanyaji wa taarifa na timu imeonekana ikipambana hivyo nitakwenda nayo sawa.”


Msimu wa 2019/20, timu hiyo ilimaliza Ligi Kuu ya Afrika Kusini ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 30.
SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII KWA SASA