Home Azam FC AZAM YAINGILIA USAJILI WA MANGALO SIMBA

AZAM YAINGILIA USAJILI WA MANGALO SIMBA

 


INAELEZWA kuwa Uongozi wa klabu ya Azam uko kwenye mipango ya kutibua mipango ya usajili ya Simba kwa kumsajili, nahodha wa klabu ya Biashara United Abdulmajid Mangalo.

Mangalo amebakiza mwaka mmoja pekee ndani ya kikosi cha Biashara United, na inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wamekuwa katika mpango mkakati wa kumsajili kwa ajili ya kuzidi kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam kimetuambia, kuwa Azam inataka kumuongeza Mangalo ili kuwa mbadala wa aliyekuwa mlinzi wa klabu hiyo, Yakubu Mohammed ambaye ni miongoni mwa nyota wanne wa kiimataifa ambao wametangazwa kuachwa na kuelekea msimu ujao.

“Ni kweli Uongozi una mpango wa kumsajili nahodha wa Biashara United, Abdulmajid Mangalo kwa ajili ya kuwa mbadala wa Yakubu ambaye klabu ilifikia makubaliano ya kuachana naye kuelekea msimu ujao wa ligi.” kimesema chanzo hicho.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ kuhusu usajili amesema: “Kwa sasa tumekamilisha asilimia kubwa ya usajili ambao tulipanga kuufanya kwa ajili ya msimu ujao.”

“Lakini hii haimaanishi kuwa hatutasajili wachezaji wengine hapana, kama kutakuwa na mapendekezo ya ziada basi tutasajili.”

SOMA NA HII  WAKATI ALEX SONG NA SOLOMON KALOU WAKIKIPIGA NA AZAM....THADEO LWANGA ATAMBULISHWA NDANI YA NYUMBA...