Home Yanga SC YANGA: MCHEZO MKUBWA HUCHEZWA NA WACHEZAJI WAKUBWA

YANGA: MCHEZO MKUBWA HUCHEZWA NA WACHEZAJI WAKUBWA


HARUNA Niyonzima, kiungo mchezeshaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa mchezo mkubwa huchezwa na wachezaji wakubwa hivyo wao hawana mashaka kuelekea mchezo wa kesho.

Kesho, Mei 8, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi ina kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes. 

Walipokutana Novemba 7 ndani ya Ligi Kuu Bara,  ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba hivyo kesho ni mchezo wa kukata na shoka. 

“Mchezo mkubwa huchezwa na wachezaji wakubwa hivyo hatuna mashaka kuhusu mchezo wetu wa kesho tupo tayari na tutapambana,” .



SOMA NA HII  BAADA YA JEMEDARI SAIDI KUTEMA NYONGO ...SHAFIH DAUDA NAYE KASHUKA NA MTU SAKATA LA YANGA NA SPORTPESA..