Home Azam FC KOCHA MPYA AZAM AANZA KAZI NA GIA KUBWA…ATAMBA KUBEBA MAKOMBE MAKUBWA AFRIKA..

KOCHA MPYA AZAM AANZA KAZI NA GIA KUBWA…ATAMBA KUBEBA MAKOMBE MAKUBWA AFRIKA..


Baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kuifundisha Azam FC, kocha mpya wa matajiri hao wa Chamazi, Mfaransa Denis Lavagne ameeleza kuanza na mbinu kali ili kuiweka timu katika muunganiko bora.

Lavagne (tamka Lavanye) ameeleza kuanza na mbinu na kuwaweka pamoja wachezaji jambo analoamini litaifanya Azam kuwa imara na kufikia malengo yake.

“Kikubwa ni kuwaweka wachezaji wote kwa pamoja, nataka waelewe mbinu zangu na kucheza kwa umoja jambo ambalo ni muhimu zaidi kwenye mpira wa miguu,” alisema Lavagne aliyepewa jukumu la kuifikisha Azam hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika na kuongeza;

“Si mara yangu ya kwanza kufanya kazi Afrika, najua ushindani uliopo na nipo hapa kuifanya Azam ifikie malengo.”

Kibarua cha kwanza cha kocha Lavagne itakuwa Jumanne ijayo katika mechi ya duru la nne ya Ligi Kuu ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Mbeya City.

Kocha huyo ana uzoefu na soka la Afrika akifundisha klabu mbalimbali pamoja na timu ya taifa ya Cameroon na mafanikio yake makubwa ni kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2008 akiwa na Cotton Sports ya Cameroon na fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2021 akiwa na JS Kabylie ya Algeria.

SOMA NA HII  GAMONDI: TULIFANYA KOSA HILI IKAWA NI ZAWADI KWA WAPINZANI