Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YAO NA FEI TOTO…..YANGA WASIMAMIA UKUCHA….WAMKUMBUSHA MAMBO YA CAS…

KUHUSU ISHU YAO NA FEI TOTO…..YANGA WASIMAMIA UKUCHA….WAMKUMBUSHA MAMBO YA CAS…

Habari za Yanga SC

Jana ilikuwa ni siku ambayo shauri la mgogoro wa Kimkataba kati ya Feisal Salum Fei Toto na timu ya Yanga SC lilikuwa linajadiliwa tena TFF kwa mara nyingine.

Pande zote mbili zilifika kwa maana ya Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick akiwa ameambatana na CEO wa Yanga Andrew Mtine lakini Feisal aliambatana na Jasmine Razack na Mwanasheria Fatma Karume maarufu kama Shangazi.

Mwanasheria wa Yanga muda mchache baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa TFF aliongea kuwa sakata hilo.

“Ni kutokuelewa sheria tu lakini ili suala lilishamalizika hapo mwanzoni, walifungua kesi mara ya pili wakaomba marejeo kilichofanyika ni kile kile tu.

“Pingamizi lulilowasilisha ni kwamba kamati ileile imeshasikiliza shauri hili mara mbili, na maamuzi ni yale yale, kwa hiyo kamati haina mamlaka tena ya kusikiliza, basi sisi tunasubiri watoe majibu ila kwa Tanzania hii kesi imeshafungwa labda waende CAS.

“Tumeshasema kama anataka kuondoka Feisal aje tumalizane vizuri ama arejee klabuni. Namhurumia kama kijana mwenzangu anapoteza kipaji chake na ajira yake,” amesema Mwanasheria Simon Patrick.

SOMA NA HII  MZIKI WA FABRICE NGOMA WAMFANYA MBRAZILI SIMBA KUIBUKA NA HILI JIPYA ...