Home Habari za michezo MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA CHAMA NA SIMBA…

MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA CHAMA NA SIMBA…

Habari za SImba SC

Clatous Chama kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba SC anapitia kipindi kigumu cha mpito kutokana na kasi yake ya kufunga kugota kwa muda mrefu akipitisha dakika 663.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele anayekipiga Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Kwenye mechi 8 za ligi ambazo alipata nafasi ya kucheza Chama hakufunga kituo kinachofauata ni dhidi ya Namungo mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Mei 3, Uwanja wa Majaliwa.

Desemba 18,2022 Uwanja wa Kirumba dhidi ya Geita Gold dakika ya 40 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa raia huyo wa Zambia kufunga.

Hakufunga Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera Sugar 1-1 Simba aliyeyusha dakika 90,KMC 1-3 Simba, Kirumba dakika 90.

Simba 7-1 Tanzania Prisons dakika 90, Uwanja wa Mkapa,Simba 3-2 Mbeya City, dakika 33, Simba 3-1 Singida Big Stars, dakika 90. Azam FC 1-1 Simba alisepa na dakika 90, Uwanja wa Mkapa.

Mtibwa Sugar 0-3 Simba alisepa na dakika 90, Uwanja wa Manungu, Simba 2-0 Yanga, Uwanja wa Mkapa alisepa na dakika 90.

Ikumbukwe kwamba ni Februari 3,2023 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Chama kugotea kutoa pasi za mwisho alipotoa mbili dakika ya 8 na ile ya 20.

Pasi zake zote hizo mbili ilikuwa kupitia mapigo huru baada ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-1 Singida Big Stars akifikisha jumla ya pasi 14 za mabao lakini idadi ya mabao ni ileile ya mwaka jana mabao matatu.

SOMA NA HII  ZA NDAAANII KABISA....MOSES PHIRI NA SIMBA MHHHH....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here