Home Uncategorized MANE ASHAURIWA KUONDOKA LIVERPOOL

MANE ASHAURIWA KUONDOKA LIVERPOOL


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Leicester City, Diomansy Kamara amemshauri nyota wa Liverpool, Sadio Mane kusepa ndani ya klabu hiyo ili kupata changamoto mpya zitakazomfanya awe bora.

Mane hesabu zake kubwa ni kupata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia (Ballon d’Or), mwaka jana alimaliza akiwa nafasi ya nne huku Lionel Messi

wa Barcelona akiitwaa tuzo hiyo.

Mane anayekipiga pia timu ya Taifa ya Senegal alijikusanyia jumla ya kura 347 huku rafikiye Mohamed Salah akiwa nafasi ya tano akiwa na kura 178.

Kamara amesema kuwa kama Mane anahitaji kweli kuipata tuzo hiyo basi ni lazima aondoke ndani ya klabu yake hiyo kwani licha ya kuwa inacheza vizuri haina uwezo wa kumtangaza zaidi.

SOMA NA HII  MAMBO YAWE MAPYA NDANI YA 2021