Home Habari za michezo RASMI…MSUVA NA RONADLO KUKIPIGA PAMOJA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

RASMI…MSUVA NA RONADLO KUKIPIGA PAMOJA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Supastaa wa Kitanzania, Simon Msuva ambaye anaichezea Al Qadsiah FC ya Saudi Arabia, itambidi kusikilizia hadi msimu ujao kuona uwezekano wa kukipiga dhidi ya mshindi mara tano wa Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo kwenye ligi kama watapanda daraja au Kombe la Mfalme, Mohammed bin Salman.

Ronaldo ambaye kwa sasa yupo midomoni mwa wadau mbalimbali wa soka kutokana na uhamisho wake ambao utamfanya kuvuna Dolla 75milion kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Sh. 175 Bilioni, amekuwa akimvutia Msuva kwa kipindi kirefu.

Licha ya kwamba ngazi ya madaraja ni tofauti, Msuva atacheza nchi moja na Ronaldo ambaye amejiunga na Al Nassr inayoshiriki ligi kuu nchini humo ambako kunasifiwa kwa wachezaji kupata maslahi makubwa ‘pochi nene’.

Msuva mwenye mabao matano kwenye Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia ambayo mzunguko wa kwanza unakaribia kumalizika, anaamini kuwa wanaweza kupanda daraja na pengine huko mbeleni anaweza kucheza dhidi ya nyota huyo.

“Ni jambo zuri kuona wachezaji wakubwa duniani kama yeye wakivutika na kuja huku hiyo inamaana kuwa watu watakuwa wakitupia macho, kwangu natazama hili kama fursa hivyo natakiwa kuongeza juhudi zaidi,” alisema.

Ronaldo ni kati wa wachezaji ambao Msuva alikuwa akiwatazama na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwake hivyo kucheza dhidi yake itakuwa historia kwenye maisha yake ya soka na hilo linaweza kutokea ikiwa chama lake litapanda daraja.

Chama la Msuva, lipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa timu 18 huku wakiwa wamekusanya pointi 16 kwenye michezo 14 wapo nyuma kwa mchezo mmoja.

Njia nyingine kwa Msuva kukipiga dhidi ya Ronaldo ni upande wa Kombe la Mfalme ambapo timu za madaraja ya chini na zenyewe hupata nafasi ya kushiriki kama ilivyo kwa Kombe la FA (ASFC) Tanzania.

SOMA NA HII  KISA TUZO ZA KINA CHAMA....SIMBA WAVIMBA NA CAF...