Home Habari za michezo BEKI HUYU KISIKI WA SIMBA ATUA NCHINI KIMYA KIMYA

BEKI HUYU KISIKI WA SIMBA ATUA NCHINI KIMYA KIMYA

Beki kutoka nchini Cameroon anayehusishwa kutua kwa Wekundu wa Msimbazi Simba Che Fondoh Malone Jr amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu nchini Cameroon kwa Msimu wa 2022/23 (2022/23 Cameroon Elite One Footballer of the Year) kwenye tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Julai 08) na Mboa Foot Awards huko Cameroon.

Beki huyo ambaye anafahamika kwa jina la utani la Ukuta wa Yericko (Wall Of Jericho) Msimu uliopita aliiwezesha timu yake ya Cotton Sports kutwaa Taji la Ligi Kuu ya Cameroon huku yeye akicheza karibia mechi zote na huku akiwa kama Nahodha wa timu.

Hata hivyo inadaiwa Beki huyo tayari ameshawasili jijini Dar es salaam Dar es salaam mapema leo alfajiri kupitia Shirika la Ndege la Ethiopia na kufichwa kwenye moja ya Hotel.

Beki huyo ambaye amechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari nchini kwao Cameroon na Tanzania anadaiwa kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kukamilisha usajili wake ndani ya Simba SC.

Young Africans yakata ngebe za usajili 2023/34 Pia inadaiwa kuwa Beki huyo anatarajiwa kufanyiwa Photoshoot ili atangazwe katika vyanzo vya habari vya Simba SC.

SOMA NA HII  BENCHIKHA HATAKI MASIHARA AWAACHA MASTAA HAWA KUELEKEA BOTSWANA ISHU NZIMA IKO HIVI