Home Habari za michezo SIKU KADHAA BAADA YA KUIKATAA YANGA SC…KWA MARA YA KWANZA FEI TOTO...

SIKU KADHAA BAADA YA KUIKATAA YANGA SC…KWA MARA YA KWANZA FEI TOTO AFUNGUKA HILI

Kiungo wa Yanga SC Fei toto akiwa anaichezea JKU jana

Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC Feisal Salum Abdallah (Fei toto) Jana Alhamis (Desemba 29) aliichezea Klabu yake ya zamani JKU dhidi ya ya Mlandege, Uwanja wa Mao Zedong kisiwani Unguja ‘Zanzibar’.

Mchezo huo wa Kirafiki umeshuhudua JKU aliyoitumikia Fei Toto kwa mara ya kwanza baada ya kuacha gumzo kwa Mashabiki wa Soka nchini Tanzania, ikiibuka na ushindi Mabao 4-2.

Kiungo huyo  alitumia dakika 45 za kipindi cha pili, ambapo aliikuta JKU ikiwa nyuma kwa Mabao 2-0, lakini uwepo wake ulisaidia kupatikana kwa ushindi huo mkubwa, huku akifunga bao moja.

Baada ya mchezo huo Mwandishi wa Habari Abubakar Kisandu alizungumza na ‘Fei Toto’, lakini alishindwa kupata ukweli wa kile alichokikusudia kutokana na muhusiska kuweka masharti ya kuulizwa swali lolote linalohusu sakata lake na Yanga SC.

“Naomba nisiongee chochote, naomba sana, ikifika siku ya kuongea nitaongea “. Alisema Fei.

Si mara ya kwanza Fei Toto kuonekana kucheza JKU kwani ndio Klabu iliyomkuza hadi alipohamia Tanzania Bara mwaka 2018, akitimkia Singida United na baadae kujiunga na Yanga SC.

Jumamosi ya Disemba 24, 2022 kupitia mitandao yake ya Kijamii Fei Toto aliwaaga Wanayanga huku timu yake hiyo siku hiyo hiyo ikitoa taarifa yakuwa bado Fei ana mkataba na Yanga mpaka Mei 30, 2024.

Hivi karibuni ziliibuka taarifa ya kuwa ‘Fei Toto’ huenda akajiunga na Azam FC kutokana na dau nono aliloahidiwa ambapo yeye binafsi aliwahi kusema hachezi mpira kufurahisha Watu bali anacheza Soka kwa kuangalia wapi kuna maslahi.

SOMA NA HII  SAMATTA: KAMA SI KIKWETE NISINGEFIKA ULAYA...NILITAKA KUJITUPA DIRISHANI KISA ASTON VILLA...