Home Geita Gold FC JAMBO LA MJAPANI WA GEITA GOLD LAFIKIA MWISHO….ISHU NZIMA IMEENDA HIVI…

JAMBO LA MJAPANI WA GEITA GOLD LAFIKIA MWISHO….ISHU NZIMA IMEENDA HIVI…

Mjapani wa Geita Gold

Baada ya kukaa nusu msimu bila kuichezea timu yake mechi hata moja ya mashindano tangu asajiliwe mwanzoni mwa msimu huu, Mjapani Shinobu Sakai wa Geita Gold yupo tayari kuwatumikia matajiri hao wa dhahabu.

Kocha mkuu wa timu Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ amekiri kushindwa kumtumia Shinobu kwenye mechi 17 za kwanza za ligi kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, lakini kwa sasa yupo tayari kucheza na atakuwa akimtumia na alianza hilo kwa kumuweka benchi kwenye mechi ya juzi dhidi ya Kagera Sugar iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

“Kuna mambo yake yalikuwa hayajakamilika, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na ndiyo maana ulimuona benchi kwenye mchezo dhidi ya Kagera. Ni kiungo mzuri na nitamtumia kwenye mechi zijazo,” alisema Minziro.

Katika mechi hiyo Shinobu alianzia benchi na katika dakika za nyongeza baada ya zile 90 za kucheza kumalizika aliinuliwa kwa ajili ya kuingia uwanjani kwa mabadiliko, lakini dakika hizo tatu ziliisha mpira bila kutoka na kujikuta akishindwa kucheza.

Huenda Shinobu akaisaidia Geita Gold kutokana na kuondokewa kwa viungo wake Yusuph Kagoma kutimkia Singida Big Stars, Saido Ntibanzokiza ‘Saido’ kujiunga Simba huku Ramadhan Chombo ‘Redondo’ akiwa mbioni kujiunga na Tanzania Prisons na Kelvin Nashoni akihitajika Simba.

Geita iliyomaliza nafasi ya nne msimu uliopita na kupata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika kwa sasa ipo nafasi ya saba kwenye msimamo na alama 24 ilizovuna katika mechi 18 ilizocheza hadi sasa.

SOMA NA HII  SAKHO, BWALYA WAUNDIWA ZENGWE CAF...SIMBA WAFICHUA JAMBO..CHAMA APEWA DK HIZI SIMBA...