Home Habari za michezo BAADA YA KUSIKIA YANGA SC WANAMTAKA…STAA WA AS VITA AIBUKA NA HILI….

BAADA YA KUSIKIA YANGA SC WANAMTAKA…STAA WA AS VITA AIBUKA NA HILI….

Tchakei Marouf kujiunga na Yanga SC

KIUNGO wa kimataifa wa Togo anayekipiga katika Klabu ya AS Vita, Marouf Tshekai ni kama amekubali kujiunga na klabu ya Yanga SC mara baada ya kuweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na timu hiyo kwa masharti.

Marouf ambaye amekuwa kiungo bora wa Ligi Kuu ya DR Congo kwa misimu miwili mfululizo ni moja kati ya wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza katika eneo la kiungo wa juu huku akiwa na sifa za kupiga mashuti ya mbali kama ilivyokuwa kwa Feisal Salum.

Kiungo huyo aliweka wazi matamanio yake ya kujiunga na timu hiyo endapo kama kila kitu kitakuwa sawa kutokana na ukubwa wa timu hiyo ambapo anaamini kuwa kila kitu kitawezekana kwake kama tu mazungumzo yatafanyika kwa pande zote tatu.

“Nimesikia juu ya Yanga SC kunihitaji, sijui zaidi kwa kuwa mimi kazi yangu ni kucheza na kwenye mambo ya usajili kama ambavyo unafahamu lazima mazungumzo ya pande tatu yafanyike kwa maana ya uongozi wangu unaonisimamia, uongozi wa timu ninayochezea na uongozi wa timu itakayokuwa inanihitaji.

“Yanga SC ni timu kubwa kwa sasa, siwezi kusema kuwa kama watanihitaji basi nitakataa lakini kikubwa ni taratibu zifuatwe kama ambavyo imekuwa utaratibu siku zote wa usajili ambavyo huwa unafanyika,” alisema kiungo huyo.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA