Home Uncategorized LIPULI: TUNAIPIGA AZAM FC NA PIPA TUNAKWEA

LIPULI: TUNAIPIGA AZAM FC NA PIPA TUNAKWEA


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wana shauku kubwa ya kukwea pipa ili kuiwakilisha nchi kimataifa hivyo kazi yao leo ni kuwakalisha wapinzani wao Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kazi ya kushinda ni ngumu hasa unapokutana na timu bora ila imani kubwa ipo kwenye ushindi.

“Najua aina ya timu ambayo tunakutana nayo ni ngumu na imewekeza kwenye mpira, ukianzia kwa wachezaji mpaka benchi la ufundi hilo halitutishi licha ya ugumu wa ratiba ambao tumepitia.

“Lengo letu kuona tunakwea pipa kuiwakilisha nchi kimataifa hilo halitakamilika kama hatutashinda ni suala la muda tu,” amesema.


Lipuli itamenyana na Azam FC leo ikiwa ni fainali ya kwanza kwake itakayochezwa uwanja wa Ilulu, Lindi.

SOMA NA HII  JESHI LA SIMBA KUIVAA AZAM FC LIMEPANGWA SIKU HII