Home news TWIGA STARS MABINGWA WA COSAFA

TWIGA STARS MABINGWA WA COSAFA


TIMU ya taifa ya Tanzania ya Wanawake Twiga Stars leo Oktoba 9 imefanikiwa kutwaa taji la COSAFA kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malawi. 

Twiga Stars imefanikiwa kutwaa taji hilo kwa ushindi wa bao pekee lililopachikwa na nyota wake Enekia Lunyamila.

Iliweza kutinga hatua ya fainali hiyo kwa ushindi wa penati 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Zambia katika nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela. 

Bakari Shime,  Kocha Mkuu wa Twiga Stars amesema kuwa ni furaha ya kila mmoja kuweza kutimiza malengo hayo.

SOMA NA HII  MAJOGORO:TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO MECHI ZILIZOBAKI