Home Uncategorized WACHEZAJI SIMBA WAPUNGUA KILO, KISA MAZOEZI SASA KAZI

WACHEZAJI SIMBA WAPUNGUA KILO, KISA MAZOEZI SASA KAZI


IMEFAHAMIKA kuwa wachezaji wote wa Simba uzito wao umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika kutokana na mazoezi mazito wanayoendelea kuyafanya.

Wachezaji hao wamefanyiwa vipimo hivyo tayari kwa kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kurejea Juni, mwaka huu mara baada ya janga la Virusi vya Corona kupungua.
Benchi la Ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ndilo lililosimamia zoezi hilo la upimwaji wa wachezaji hao kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinaeleza kuwa katika vipimo hivyo walivyofanyiwa mastaa hao, wote walionekana kupungua uzito kati ya kilo 4-5 na kugundulika walifanya mazoezi kwa kiwango kikubwa.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa baada ya kugundulika wachezaji hao uzito wao umepungua, viongozi hao wa benchi la ufundi wanafi kiria jinsi ya kuwarejeshea uzito wao uliopungua.

Aliongeza kuwa, mara baada ya ligi kusimama, wachezaji wote walipewa programu maalum za mazoezi na kocha wao, Sven akiwataka kuzifuata ili kuhakikisha viwango vyao havishuki.
“Wachezaji wamefanyiwa vipimo juzi na wote wamegundulika uzito wao umepungua, hivyo hivi sasa viongozi wanafanya juu chini kuweza kuwarejeshea uzito wao uliopungua.
SOMA NA HII  NYOTA AZAM FC APANIA KUFANYA VIZURI