Home Uncategorized NYOTA AZAM FC APANIA KUFANYA VIZURI

NYOTA AZAM FC APANIA KUFANYA VIZURI

MBARAKA Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa yupo kamili fiti kuendelea kupambana ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Aristica Cioaba, raia wa Romania.
Mbaraka alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti aliyokuwa akiyatibu aliyapata akiwa ndani ya Namungo FC msimu wa 2018/19 alipokuwa akicheza kwa mkopo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mbaraka amesema kuwa kwa sasa ni suala la muda tu yeye kuonekana uwanjani.
“Nipo fiti kwa sasa iwapo nitapata nafasi ya kucheza nitafanya vizuri kwenye mechi zetu kwani suala la kuanza lipo mikononi mwa kocha,” amesema.
Azam  FC ipo nafasi ya pili kibindoni ina pointi 57 imebakiza mechi 9 kumaliza mzunguko wa pili.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA MBAO KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA YANGA UWANJA WA TAIFA