Home Uncategorized YANGA YAMVUTA KIKOSINI NYOTA HUYU WA MTIBWA SUGAR

YANGA YAMVUTA KIKOSINI NYOTA HUYU WA MTIBWA SUGAR

NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa iwapo Yanga itamalizana na beki wa pembeni, Kibwana Shomari anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar watakuwa wameongeza mtambo wa kazi.
Imekuwa ikielezwa kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kumnasa beki huyo ambaye aliwapa tabu Simba kwenye mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi ambalo Mtibwa walisepa nalo kwa kuitungua bao 1-0 Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul alisema kuwa ikiwa Yanga watamalizana na Shomari anaamini itaongeza uimara ndani ya kikosi.
“Shomari ni miongoni mwa mabeki ambao wanafanya vizuri ndani ya uwanja, bado sijaskia kwamba anaweza kujiunga kikosini ila ikiwa itatokea akaja Yanga basi kikosi kitazidi kuwa imara zaidi.
“Kwa mabeki wazawa, kijana anajitahidi kwani anajua kutumia vizuri nafasi yake akiwa ndani ya uwanja na ni mtulivu, akiwa makini zaidi atafika mbali na akija hapa Yanga nitampa ushirikiano mkubwa,” amesema Abdul.
SOMA NA HII  VIDEO:UWANJA WA KISASA ULIOJNGWA SHINYANGA ACHA KABISA