Home Uncategorized AZAM FC, SIMBA WAMKUMBUKA PATRICK MAFISANGO

AZAM FC, SIMBA WAMKUMBUKA PATRICK MAFISANGO


PATRICK Mafisango mchezaji wa zamani wa Simba na Azam FC tarehe kama ya leo alitangulia mbele za haki kwa kupata ajali.

Timu zote mbili Azam na Simba zimemlilia nyota huyo ambapo Azam FC kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika namna hii:-“Julai 14, 2010 tulimsajili Patrick Mutesa Mafisango kutoka APR ya Rwanda.

“Usajili wa Mafisango uliambatana na wachezaji wengine kama Mohamed Binslum (Huru) Jackson Chove (JKT Ruvu), Jabir Aziz  na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Simba), Mrisho Ngassa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling ‘Kali Ongala’ (GIF-Sweeden) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda.)

“Aprili 2011, Mafisango akapelekwa kwa mkopo Simba SC kwa maelekezo ya kocha wetu, Stewart John Hall, ambaye alimtaka Abdulhalim Humud kutoka Simba.

“Kocha Stewart alishawahi kufanya kazi na Humud akiwa timu ya taifa ya Zanzibar.

“Tarehe kama ya leo, 2012, Mafisango alifariki dunia.

Tarehe kama ya leo miaka nane iliyopita aliyekuwa kiungo wetu Patrick Mafisango alifariki dunia kwa ajali ya gari. Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza roho yake mahala pema peponi,”.

Kwa upande wa Simba kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika namna hii:”Tarehe kama ya leo miaka nane iliyopita aliyekuwa kiungo wetu Patrick Mafisango alifariki dunia kwa ajali ya gari. Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza roho yake mahala pema peponi,”.

SOMA NA HII  NYOTA WA AFRIKA WANAOKIPIGA PREMIER KATIKA NAMBA NA MABAO WALIYOPACHIKA KWENYE TIMU ZAO ZA TAIFA