Home Uncategorized WINGA AS VITA AKUBALI KUTUA YANGA

WINGA AS VITA AKUBALI KUTUA YANGA


WINGA machachari wa AS Vita, Tuisila Kisinda, amesema kuwa Yanga ndiyo timu ambayo ipo akilini mwake baada ya kufanikiwa kufanya mazungumzo ya awali na uongozi wa timu hiyo.
Yanga SC katika kuhakikisha inakijenga kikosi chao kuwa imara, imeahidi kuleta majembe kutoka timu zinazofanya vizuri katika michuano ya kimataifa kama AS Vita na timu nyingine.
Kisinda amesema kuwa kuna mazungumzo ambayo alifanya na kiongozi mmoja wa Yanga ambayo yanamfanya azidi kuifi kiria zaidi timu hiyo ambayo imeonyesha nia ya kumhitaji winga huyo.
“Nilifanya mazungumzo na mmoja wa viongozi wa Yanga, japo hatukukamilisha mipango yote ya usajili, hivyo maongezi hayo yananifanya nizidi kuifikiria Yanga kwa kuwa wana mpango na mimi wa kunisajili.
“Kama kila kitu kitaenda sawa huko mbeleni nadhani nitatua kwenda kucheza Yanga, kiufupi napapenda sana Tanzania kwa kuwa watu wake wanapenda amani na watulivu sana, navutiwa zaidi kucheza kwao kama nitafanikiwa,” amesema winga huyo.
SOMA NA HII  MABOSI WA YANGA WAMALIZA UTATA KUHUSU MORRISON