Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA WAARABU WA IBENGE JUZI…PABLO NA SIMBA YAKE WACHUKUA...

BAADA YA KUMALIZANA NA WAARABU WA IBENGE JUZI…PABLO NA SIMBA YAKE WACHUKUA MTAZAMO HUU…


LICHA ya Simba kuongoza kundi ‘D’ la Kombe la Shirikisho Afrika na pointi saba baada ya kuifunga RS Berkane bao 1-0, ila kocha, Pablo Franco ameelekeza nguvu zake katika mchezo mgumu ugenini dhidi ya Asec Mimosas, Jumapili ijayo.

Pablo alisema; “Tulihakikisha Berkane hatuwapi nafasi kwenye mipira ya kutenga kwa kuweka watu wa kuzuia na tuliwafanya kukosa mbinu mbadala na kutufanya kuwa salama zaidi, pia udhaifu wao hasa upande wa beki ya kushoto ulitusaidia kuutumia na tulifanikiwa.”

“Kila mchezo lazima tucheze kwa malengo tunajua Asec haitokuwa mechi rahisi kulingana na tofauti ya pointi zilizopo hivyo ni lazima kucheza kwa tahadhari na kwa umakini mkubwa,”aliongeza.

Kutokana na kukosekana kwa kiungo Mzambia, Clatous Chama katika michezo ya kimataifa kulingana na taratibu za kikanuni, Pablo ameamua kuwatumia mastaa wake Pape Ousmane Sakho aliyefunga mechi iliyopita , Bernard Morrison na Rally Bwalya kwa ajili ya kubeba majukumu hayo.

“Kocha yeyote anapenda uwepo wa wachezaji wake wote muhimu kikosini, lakini hilo haliwezi kutotoa mchezoni na tukatetereka kwa sababu tuna wachezaji bora ambao wanaweza kucheza eneo hilo na kutuhakikisha tunapata matokeo chanya tunayohitaji.”

Jeuri nyingine ya Simba ni rekodi nzuri iliyonayo katika mechi za ugenini kwani katika kundi hilo ndiyo timu pekee iliyotoa sare ugenini 1-1 dhidi ya US Gendarmarine Februari 20, pia kama haitoshi ndiyo timu pekee iliyoruhusu mabao machache (matatu), ugenini tofauti na wengine, ikianza na 1-1, dhidi ya US Gendarmarine, kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa RS Berkane Februari 27.

SOMA NA HII  KUHUSU ALIPO CHIKO USHINDI NA UWEZO WAKE UWANJANI..NABI ATOA SABABU NYINGINE....ATANGAZA VITA...