Home Habari za michezo KISA KUIITA LIGI YA TZ DHAIFU…MANARA AMSHUKIA JUMLA JUMLA AHMED ALLY…AFICHUA YA...

KISA KUIITA LIGI YA TZ DHAIFU…MANARA AMSHUKIA JUMLA JUMLA AHMED ALLY…AFICHUA YA WASAUZI…


Baada ya Siku ya Jana Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally kuchapisha andiko katika ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa Ligi ya Tanzania ni dhaifu kutokana na kuwa na timu nyingi ambazo zinagombea kushuka daraja badala ya Ubingwa.

Aidha Ahmed alikwenda mbali pia na kuainisha wakati Ligi imefika mzunguko wa 22 ni timu tatu tu ambazo zimefikisha alama 30 na zaidi.

Sasa Msemaji wa Klabu ya Yanga na Vinara wa Ligi Kuu Bara, Haji Manara amemuwashia moto Afisa Habari huyo wa Simba ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagrama Manara ameandika;

“Kama ligi yetu ni dhaifu why team yako isiwe inaongoza wakati imetoka kumfunga Orlando na Berekane wanaocheza hizo ligi ngumu?

Au tuamini yale maneno ya Team ngeni zinazokuja kucheza na nyinyi,,ya kwamba mnawawekea mifamba yenu katika misosi na vitoa upepo?

Ligi yetu kama ni dhaifu Kwa nini mlisema mnamaliza mambo ya CAF kisha mnakuja kuchukua ubingwa wenu,.ilhali hadi sasa team lenu lipo nyuma kwa Points kumi na tatu?

Inafikirisha vp ufungwe na kagera kisha udroo na Mtibwa na kina Coastal wanaoshika mkia,,halaf umfunge Asec? Au ndio hzo 4 4 2 zenu?

Ligi hii dhaifu sawa kwa kuwa hamshindi ubingwa Nyie,,vp na ww sio dhaifu kwa kuongea huku unabana bana pua?

Tuwe na heshma kwa investment iliyowekwa na Azam na Sponsors wengine, leo hakuna team inahangaika na nauli wala mishahara ya Wachezaji,,leo Ligi ya Tanzania hadi anaeshuka daraja atavuta mzigo,

Udhaifu ni wenu kwa team lenu ambalo so far inaweza hata kushuka daraja ikipoteza mechi zilizobakia,,

Kisa Yanga anachukua ubingwa ndio ligi dhaifu,,ila mngekuwa mnachukua nyie ligi ingekuwa ngumu sio?”

SOMA NA HII  KUHUSU TIMU GANI ATAICHEZEA MSIMU UJAO...DILUNGA AIKANA SIMBA...AIITA YANGA MEZANI...