Home Simba SC KUELEKEA MECHI YA KESHO: GOMES ‘AVIMBA’ NA UWEPO WA NYONI NA KENNEDY

KUELEKEA MECHI YA KESHO: GOMES ‘AVIMBA’ NA UWEPO WA NYONI NA KENNEDY


UWEPO wa mabeki wa kati, Erasto Nyoni na Kennedy John umempa jeuri kocha wa Simba, Didier Gomes katika mchezo wao wa hatua ya makundi kwenye Ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merikkh.

Simba Jumanne Machi 16, 2021 itakuwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Merikkh mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni.

Katika mchezo huo Simba itawakosa nyota wake watatu, Ibrahim Ame (majeruhi), Taddeo Lwanga na Pascal Wawa ambao wana kadi mbili za njano.

Akizungumza mara  baada ya mazoezi kumalizika, Gomes alisema licha ya kuwakosa nyota hao anaamini ana wachezaji wengine watakaoziba pengo lake.

“Nitamkosa Ame mwenye majeruhi kidogo na Wawa lakini nina Nyoni na Kennedy ambao mpaka mazoezi ya kesho tutajua nani atacheza”.

Pia wachezaji hao katika mazoezi ya leo jioni walikuwa wanaonyesha utulivu katika ukabaji pamoja na kuanzisha mashambulizi na sio kubutua.

SOMA NA HII  BOCCO NAYE AONGEZA MIAKA MIWILI YA KUSALIA MSIMBAZI