Home Uncategorized SABABU ZA NYOTA WA YANGA KUIBUKIA GWAMBINA YAWEKWA WAZI

SABABU ZA NYOTA WA YANGA KUIBUKIA GWAMBINA YAWEKWA WAZI


 MABAO 25, ndani ya kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars ni sababu kubwa ya Klabu ya Gwambina kuvutiwa na mpango wa kumsajili nyota wa zamani wa Klabu ya Yanga, Mrisho Ngasa.

 

Ngasa anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ndani ya kikosi cha Stars kwa wachezaji wa kizazi cha sasa akiwa ameweka kambani mabao 25, akizidiwa mabao matatu tu na mfungaji bora wa muda wote ndani ya kikosi hicho, Sunday Manara ambaye ana mabao 28.


Ngassa alikuwa sehemu ya wachezaji 14 walioachwa na Yanga Agosti 3, mwaka huu.


Mratibu wa Mashindano wa Gwambina, Mohamed Almas alisema usajili wa nyota huyo ni mapendekezo ya Kocha Mkuu, Fulgence Novatus na Mkurugenzi wa Ufundi, Mwinyi Zahera.

 

“Suala la usajili wa Ngassa limekamilika kwa kiwango kikubwa, usajili wake ni mapendekezo ya Kocha Novatus ambao umethibitishwa na mkurugenzi wetu wa ufundi, Zahera.

 

“Kimsingi tunatarajia matokeo makubwa baada ya kukamilisha usajili huu, kwa kuwa Ngassa ni mchezaji mkubwa na hata takwimu zinambeba ambapo mpaka sasa ni mfungaji bora wa muda wote wa Stars kwa vizazi vya sasa akiwa amefunga mabao 25, lakini hata mchango wake kwenye mafanikio ya klabu nyingine ni mkubwa,” alisema.

 

Gwambina ina pointi 19 baada ya kucheza mechi 16 mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Gwambina watakosa huduma ya nahodha Jacob Masawe kwa kuwa ana kadi tatu za njano.


Mchezo huo ni wa kwanza kwa mwaka 2021 ambao unatarajiwa kuchezwa Januari 3.

SOMA NA HII  HAPA NDIPO WALIPOPISHANA JEMBE NA MAREHEMU RUGE