Home Uncategorized MKWANJA ANAOVUTA KAZE WAMPOTEZA SVEN WA SIMBA

MKWANJA ANAOVUTA KAZE WAMPOTEZA SVEN WA SIMBA

 


UKIWEKA kando ishu ya kuwa namba moja ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya timu yake kucheza jumla ya mechi 17 na kibindoni kukusanya pointi 43, Cedric Kaze amewapoteza makocha wengine Bongo kwa mkwanja.


Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu, Kaze anapokea mshahara mkubwa kuliko makocha wengine ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Anatajwa kuvuta kiasi cha dola 10,000 (zaidi ya milioni 22) ambazo zinatolewa na mdhamini wao Bilionea Gharib Said Mohamed (GSM).


Unaambiwa hiyo ni mshahara pekee achana na marupurupu pamoja na bonasi ambazo anazipokea pale timu inaposhinda ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za FA ambazo bado hajaanza kucheza.


Anafuatiwa na Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ambaye inatajwa kuwa analipwa dola 9,000 sawa na milioni 20 za kibongobongo.


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  HUO MKWARA WA SIMBA KWA ASEC SIO POA