Home Uncategorized WILFRIED ZAHA AINGIA ANGA ZA AC MILAN

WILFRIED ZAHA AINGIA ANGA ZA AC MILAN

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya AC Milan inayoshiriki Serie A inahitaji saini ya Wilfried Zaha wa Crystal Palace. 


Winga huyo mwenye miaka 28 amekuwa kwenye rada za timu nyingi ambazo zinahitaji saini yake huku Milan wakipewa chapuo kupata saini yake.


Milan imani yao ni kwamba ikiwa watapata saini ya nyota huyu ataongeza makali ya kuwania taji la Serie A ambalo wanalihitaji kabisa.


Kwa mujibu wa Gazeti la The Sun, Zaha anataka kuondoka ndani ya timu hiyo ili akapate changamoto mpya.

SOMA NA HII  BEKI KISIKI NDANI YA INTER MILAN AIPIGIA HESABU MANCHESTER UNITED