Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA…HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUENDELEA NA ...

KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA…HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUENDELEA NA MGUNDA…

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wana imani kubwa na Kocha Juma Mgunda kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans.

Miamba hiyo ya Kariakoo-Dar es salaam inatarajia kukutana Jumapili (Oktoba 23) Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Young Africans wakiwa mwenyeji.

Ahmed Ally ameweka wazi kuwa na imani na Kocha Mgunda alipohojiwa na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, kuhusu mchezo huo, ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Soka la Bongo.

Ahmed ally amesema: “Wenzetu hii mechi ndio Kombe la Dunia kwao, hii mechi ndio mafanikio yao… Mashabiki wanatoa macho, viongozi wanatoa macho na wachezaji wao wanatoa macho,”

“Kwa hiyo unapokutana na timu inayokamia mechi moja inakupa ugumu kidogo ila bahati nzuri tunae Juma Mgunda,anajua kuzicheza mechi hizi..Naamini tutahakikisha tunapata alama 3”

Mara ya mwisho timu hizo zilipokuatana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 2-1, mabao ya Young Africans yakifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele, huku Pape Ousmane Sakho akiifungia Simba bao la kufutia machozi.

Msimu uliopita katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara timu hizo hazikufungana, baada ya kutoka suluhu.

SOMA NA HII  HII HAPA KAULI YA GAMONDI BAADA YA KUONA UWEZO WA OKRAH..."ATAPISHA WENZAKE"....