Home Habari za michezo HII HAPA KAULI YA GAMONDI BAADA YA KUONA UWEZO WA OKRAH…”ATAPISHA WENZAKE”….

HII HAPA KAULI YA GAMONDI BAADA YA KUONA UWEZO WA OKRAH…”ATAPISHA WENZAKE”….

Habari za Yanga leo

AUGUSTINE Okrah ‘Okrah Magic’ tayari ni mali ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi juzi Jumapili usiku wa kuamkia Mwaka Mpya 2024. Sasa unajua Kocha Miguel Gamondi amefunguka nini kuhusu mchezaji huyo?

Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Ghana ametua Yanga akitokea Benchem na usajili wake na Gamondi amefunguka hana wasiwasi nao lakini atatakiwa kuonyesha ubora wake ili awe na nafasi kikosini.

Gamondi amefunguka hayo baada ya utambulisho wa mchezaji huyo, wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa kwanza wa mashindano ya Mapinduzi wa mabao 5-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Okrah ana kazi kubwa ya kufanya kumshawishi Gamondi ambaye mwenyewe alisema uongozi umemfuatilia mchezaji huyo kwa miezi miwili na kubaini ubora wake hivyo anaamini ataisaidia timu hasa kipindi hiki wana mashindano mengi.

“Sina wasiwasi na usajili wa Okrah kwa sababu ni mchezaji ambaye ana uzoefu na ligi ya Tanzania na rekodi zake alipotoka kitakwimu ni nzuri, pia uongozi kabla ya kumsajili umemfuatilia Kwa miezi miwili naamini atakuwa msaada kwenye kikosi,” alisema.

“Sihitaji kuzungumza mambo mengi sasa kuhusu mchezaji huyo, nitampa nafasi aonyeshe kwa vitendo ubora wake, utakaompa nafasi ya kucheza zaidi, akishindwa kufanya kile tunachokitarajia kutoka kwake atawapisha wengine wacheze,” alisema.

Gamondi alisema dirisha hili la usajili ni bahati kupata mchezaji mzuri kutokana na wengi kuwa na mikataba na timu zao na kuivunja ni gharama kubwa.

Gamondi ambaye sio muumini wa kutumia wachezaji wa pembeni (winga) ana kibarua kuhakikisha anampa nafasi mshambuliaji huyo ambaye anamudu pia kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji ambayo kwa sasa ina watu na wanafanya vizuri.

Eneo hilo kwa sasa wanacheza StephanE Aziz KI ambaye ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akiwa nayo 10, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.

Yanga chini ya Gamondi haijawapa nafasi mawinga, Jesus Moloko na Farid Musa ambao wanatokea pembeni kutengeneza mashambulizi, tofauti na ilivyokuwa chini ya Kocha Nasreddine Nabi.

Okrah aliyewahi kuichezea Simba lakini hakufanya vizuri, ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga dirisha hili, baada ya kiungo kutoka JKU, Shekhan Ibrahim Hamis na sasa wanapambana kusaka mshambuliaji namba tisa atakayeziba pengo la Fiston Mayele aliyetimka msimu uliopita.

SOMA NA HII  SABABU ZA TAIFA STARS KUWANIA TUZO ZATAJWA.......CAF YAWEKA KILA KITU HADHARANI