Home Habari za michezo WAKATI HUKUMU ZAO NI KESHO….KAPAMA NA SIMBA WAMALIZANA KIMYA KIMYA..CHAMA MHHH…

WAKATI HUKUMU ZAO NI KESHO….KAPAMA NA SIMBA WAMALIZANA KIMYA KIMYA..CHAMA MHHH…

Habari za Michezo leo

JAPOKUWA inaelezwa kwamba tayari kwa upande wa maamuzi wa kiraka wa Simba, Nassoro Kapama ni kuachana naye, kesho Jumatano kutafanyika kikao cha kuwajadili na mwenzake Clatous Chama.

Wawili hao walisimamishwa na uongozi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu, hivyo kesho ndiyo hatima rasmi itafahamika kama wanarudi kikosini au wanaondolewa jumla

Hata hivyo kutokana na Chama kuwa nchini kwao Zambia na timu ya Taifa ya nchi hiyo inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika Afcon kikao hicho kitafayika kwa kutumia teknolojia ya kimataifa ya zoom.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kinasema :”Simba kwa sasa inahitaji nidhamu kwa kila mfanya kazi, ili kurejea kwenye ushindani na uwanjani kuonyesha kiwango cha juu, kitakachowapa mashabiki furaha na siyo vidonda vya tumbo.

“Angalau ujio wa kocha unaanza kuwarejesha kwenye mstari, sasa hatutaki ndani ya timu kusikike mara mchezaji huyu kafanya hivi, mara yule kile, hayo kwa sasa yanakwenda kufikia mwisho.”

Kuhusiana na Chama: Jumatano kikao kitaamua kama msimu huu uwe wa mwisho kwake baada ya kutumikia timu hiyo tangu alipojiunga nayo msimu 2018, akitokea klabu ya Power Dynamos na baadaye kutimkia RS Berkane ambapo hakuchukua muda akarudi tena Tanzania, sijafahamu nini kitatokea, tusubiri tuone.

Wakati huohuo baada ya kumaliza kikao cha kuwajadili Chama na Kapama ambaye chanzo kinasema kuwa tayari kwa aslimia kubwa hana maisha ndani ya timu hiyo na kesho ni kama kumalizia tu, kamati ya usajili itakutana kujadili ni wachezaji gani wanapaswa kuwaongeza na kuwaondoa ndani ya timu.

“Kabla ya dirisha kufungwa kila kitu kitakuwa sawa, pia watakaondoka tunatoa nafasi ya wao kusaka timu za kuzichezea mapema,”alisema.

SOMA NA HII  HUKO SIMBA MAMBO YANAZIDI KUNOGA, NAFASI YA MANULA YACHUKULIWA NA MCAMEROON, HUKU MASTAA WENGINE WANNE WATUA SIMBA