Home Habari za michezo SABABU ZA TAIFA STARS KUWANIA TUZO ZATAJWA…….CAF YAWEKA KILA KITU HADHARANI

SABABU ZA TAIFA STARS KUWANIA TUZO ZATAJWA…….CAF YAWEKA KILA KITU HADHARANI

Taifa Stars

ACHANA na rekodi za nyuma. CAF wametaja klabu 10 kubwa kwa sasa zinazowania tuzo ya klabu bora ya mwaka 2023 Afrika. Tanzania imeingia Yanga ya Kocha Miguel Gamondi tu.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jana lilitangaza timu na wachezaji ambao watawania tuzo za ubora 2023 huku Yanga ikitoa pia kipa bora na mchezaji bora anayewania tuzo kwa mwaka huo ambao walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho ikiwa na rekodi nzuri Afrika.

Klabu zingine zinazowania tuzo hiyo na Yanga ni Mamelodi Sundowns, Marumo Gallants (Afrika Kusini), Al Ahly (Misri), Wydad AC na Raja CA (Morocco), USM Alger na CR Belouzdad (Algeria), ASEC Mimosas (Ivory Coast), ES Tunis (Tunisia).

Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kuwania tuzo hiyo ya timu bora ya mwaka ambayo itatolewa Desemba 11, jijini Marrakech Morocco huku baadhi ya mashabiki wakishtushwa na Simba kutotokea kwenye tuzo hizo kama klabu au kuingiza hata staa wake yoyote kwenye kipengele chochote. Yanga inaendelea kuonyesha heshima yake baada ya msimu uliopita kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini bahati haikuwa yao baada ya USM Algier kutwaa ubingwa huo kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya mabao 2-2, ikikosa ubingwa kikanuni.

Yanga ambayo kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 18, tayari imeshafuzu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ipo kundi moja ya timu Al Ahly, Belouzdad na Medeama ya Ghana.

Kipa Djigui Diarra na aliyekuwa mshambuliaji wao msimu uliopita Fiston Mayele anayekipiga Pyramids ya Misri wameteuliwa kwenye nafasi zao.

Mbali na hao tuzo hiyo pia inawaniwa na mastaa wengine 20 akiwemo Pecy Tau, Ranga Chivaviro, Peter Shalulile, Mohamed ElShenawy na wengine wengi kutoka kwenye timu kubwa Afrika.

Kutokana na ubora wa Diarra, ameingia pia kwenye vita ya kuwania tuzo ya kipa bora ya mwaka ambayo imemhusisha staa anayecheza Man United, Andre Onana raia wa Cameroon, yumo Mohammed El Shenawy wa Al Ahly, Edouard Mendy Al AHli ya Saudia, Oussama Benbot, Pape Mamadou, Landing Badji, Yassine Bounou, Ronwen Williams na Yassine Bounou.

Mchezaji pekee ambaye amewahi kuiheshimisha nchi kwenye tuzo kama hizi ni Mbwana Samatta ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayecheza ligi ya ndani akiwa anaitumikia TP Mazembe mwaka 2016.

TIMU BORA YA TAIFA

Cape Verde, Gambia, Guinea Bissau, Guinea ya Ikweta, Mauritania, Morocco, Msumbiji, Namibia, Senegal na Tanzania. Kwa mujibu za CAF, Tanzania imeingia kwenye timu za Taifa kutokana na ufanisi wake wa tangu mwaka jana kwenye michuano mbalimbali.

Nyota wa zamani wa Mecco, Abeid Kasabalala, alisema katika tuzo hizo wanaowania ambaye ni Diarra na Mayele wote wanatoka mataifa ya kigeni hivyo wazawa wapambane kuhakikisha wanakuwa sio tu ndani mpaka Afrika.

Staa wa zamani wa Yanga, Abel Mziba alisema tuzo hizo zinaashiria soka la Tanzania linakuwa kwa kiasi kikubwa huku wageni wakitawala zaidi na ni funzo tosha kwa wachezaji wa ndani kupambana.

SOMA NA HII  KISA GOLI LA BIASHARA UTD JUZI....MABEKI YANGA KUKIONA CHA MOTO...KAZE AAPA 'KULALA NAO MBELE.'...