Home Uncategorized SONSO YUPO TAYARI KWA MAPAMBANO NDANI YA LIGI KUU BARA

SONSO YUPO TAYARI KWA MAPAMBANO NDANI YA LIGI KUU BARA

BEKI wa Yanga, Ally Mtoni ‘Sonso’ amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mapambano ndani ya Ligi Kuu Bara kumaliza mechi zilizosalia ndani ya msimu wa 2019/20.

Masuala ya michezo yalisimamishwa na Serikali, Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea Juni Mosi baada ya Serikali kusema kuwa hali imeanza kuwa shwari.

Sonso amesema kuwa wakati wa mapumziko ya lazima alikuwa anafanya mazoezi binafsi hivyo anaamini bado anaweza kuhimili mikiki ya ndani ya Uwanja.

 “Nilikuwa ninafanya mazoezi binafsi hivyo hainipi tabu kurejea kwenye mechi za ushindani imani yangu kwamba nitafanya vizuri na kwa kushirikiana na wenzangu tutapata matokeo chanya. 

“Kikubwa sapoti na kusubiri kuona mambo yatakavyokuwa kukaa bila kucheza tulikuwa tumekumbuka mpira,” amesema.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA