Home news YANGA:TUTARUDI TUKIWA IMARA ZAIDI

YANGA:TUTARUDI TUKIWA IMARA ZAIDI


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa utarejea ukiwa imara kwa ajili ya mchezo wa marudio dhidi ya Rivers United unaoatajiwa kuchezwa Nigeria, Septemba 19.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilipoteza mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwa kukubali kuona ubao ukisoma Yanga 0-1 Rivers, United.

Mchezo wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kwa kuwa kila timu inasaka ushindi.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa wananafasi ya kufanya kwa ajili ya dakika 90 zilizobaki huku akiwaomba mabashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwa bega kwa bega.

Pia kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa Yanga wameandika ujumbe huu:”Jumapili hii ya 19/9/2021, tunashuka dimbani kwenye mchezo wetu wa marudiano wa kimataifa hatua ya awali dhidi ya Rivers United FC nchini Nigeria.


“Tutarudi tukiwa imara zaidi,” .

SOMA NA HII  SIKU KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA AL AHLY...BENCHIKHA KAJA NA 'PIGO' HILI MATATA....